Jumatatu, 2 Desemba 2013

FOMU YA KUJIUNGA NA MTWANGO SEKONDARI



                                  NJOMBE DISTRICT   DEVELOPMENT TRUST
                                            EDUCATION   DEPARTMENT
                                  SHULE YA SEKONDARI MTWANGO
                                               S.L.P 370. NJOMBE
                                               mtwaseco@gmail.com
                                Simu: +255756962462(mkuu wa shule)

Kumb.Na.MTSS/AD.I/VoIV/75



        YAH: MAAGIZO YA KIJIUNGA NA SHULE YA SEKONDARI MTWANGO

UTANGULIZI
Ninayo furaha kukuarifu kuwa umechanguliwa  kujiunga na kidato cha……katika shule hii kuanzia tarehe……..Hii ni bahati kubwa Sana kwako.Nimatumaini  yangu kuwa utaitumia vizuri nafasi hii kwa manufaa yako mwenyewe,wazazi wako na taifa kwa ujumla.
Hii ni ya kutwa na ina hosteli.Utaishi nyumbani kwa mzazi au shuleni kwenye hosteli.Jaza fomu ya kukubali nafasi hii wewe na mzazi au mlezi wako.
Nenda Kwa daktari wa hospitali iliyo jirani nawe ili ukapimwe afya yako na kurudisha cheti cha Daktari hapa shuleni siku ya kujisajili
Nunua vifaa vyote muhimu ulivyoagizwa

A:MAHITAJI MUHIMU YA SHULE
  (1)Wasichana
  (a)Blauzi nyeupe mikono mifupi (2)
  (b)Soksi nyeupe jozi mbili (2)
  (c)Sketi mbili (2) rangi ya bluu bahari kitambaa kizito kwa ajili ya kuvaa wakati wa vipindi (darasani) mshono marinda nchi tatu (3) sketi ivuke magoti
  (d)Sketi mbili rangi ya pinki za heshima Kwa ajili ya kuvaa baada ya vipindi kwa wale wa hosteli
  (e)Tisheti mbili (2) rangi ya njano zisizo na maandishi
  (f)Sweta mshono V isiyo na maandishi iliyoshonwa kwa uzi wa rangi ya kijani kibichi
  (g)Viatu vya jozi moja, rangi nyeusi, visigino vifupi visivyo vya wazi
  (h)Raba ya michezo jozi moja
  (i)Bukta moja na fulana yake (rangi yoyote) kwa ajili ya michezo
  (j)Fyekeo moja
  (k)Sketi mbili (2) kitambaa kizito rangi ya kijani kibichi(kwa wanafunzi wa kutwa),mshono marinda nchi tatu(3)ivuke magoti
  (l)Track suits rangi ya Bluu yenye “strips”nyeupe mikononi.

(2) Wavulana
(a)Mashati mawili meupe mikono mifupi.
(b)Suruali za heshima mbili (2) rangi nyeusi, mifuko mitatu kwa ajili ya kuvaa wakati wa darasani.
(c)Suruali za kushona mbili (2) rangi ya khaki, za kuvaa baada ya vipindi
(d)Sweta mshono V isiyo na maandishi rangi ya bluu iliyokolea
(e)Viatu vya ngozi jozi moja, rangi nyeusi na visigino vifupi visivyo vya wazi
(f)Raba ya michezo jozi moja
(g)Bukta moja na fulana yake (rangi yoyote) Kwa ajili ya michezo
(h)Jembe moja lenye mpini
(i)Suruali mbili (2) za heshima rangi ya kijani kibichi (kwa wanafunzi wa kutwa) mifuko mitatu kwa ajiri ya kuvaa wakati wa darasani
(j)Tisheti mbili (2) rangi ya njano zisizo na maandishi
(k)Track suits nyeusi yenye “strips”nyeupe mikononi.


WOTE:

B: ADA
Ada ya mwaka ni shilingi milioni moja tu(Tsh.1,000,000/=) kwa hosteli. Wale wa  kutwa  ni  laki  sita  na  nusu tu  (650,OOO/=)

C: MICHANGO:
i).MCHANGO WA MAJI, MAJENGO, UMEME NA INTERNET TSH 60,000/=

ii).FEDHA  YA  TAHADHARI (CAUTION  MONEY) 
Uje  na  shilling  elf   kumi(Tsh 10,000/=)  kwa  ajili  ya tahadhali(caution  money)

iii.)KITAMBULISHO CHA SHULE
Uje na shilling elfu tano tu (5,000/=) kwa ajili ya kitambulisho
Picha  mbili  ndogo(passport  size)  kwa  ajili  ya matumizi  ya shule.

iv).MITIHANI
Uje  na bunda   moja  ya  karatasi  kwa  ajili  ya  majaribio  na mitihani  ya  ndani(photocopy  A4 size)

v).CHAKULA (Kwa wale wa hosteli tu)
uje  na  sahani,kikombe  na kijiko  kwa  ajili  ya  chakula

vi).MALAZI (Kwa wale hosteli tu)
Uje na:
a)Godoro  la  upana  wa   futi  mbili  na nusu  na mto  mmoja
b) Blanketi zito Mtwango ni eneo la baridi. Pia mashuka mawili: Wasichana rangi PINKI na wavulana rangi ya BLUU.
c).Taulo
d).Ndoo

vii).WANAFUNZI   WA KUTWA NI WAZAWA MTWANGO TU.


viii).KURIPOTI SHULENI:
Unatakiwa kuripoti shuleni tarehe..............................…, saa nne(4.00)asubuhi.
Ili  upokelewe  unatakiwa uje  na  vifaa/mahitaji  yote  yaliyo  orodheshwa  hapo  juu  pamoja  na  stakabadhi  ya  benki(banki  pay –in slip) isiyopunguwa shillingi:
  • LAKI TANO NA ELFU  SABINI  NA  TANO(575,000/=)KWA  WANAFUNZI WA  HOSTELI,
Kwa muhula wa kwanza, 500,000/=muhula wa pili
  • LAKI NNE(400,000/=) kwa  muhula wa kwanza,325,000/=kwa  muhula  wa pili  kwa  WANAFUNZI  WA  KUTWA.


Malipo yote yafanywe benki kwenye akauti zifuatazo
                  1. NBC
                   MTWANGO SECONDARY SCHOOL
                   ACCOUNT   NO.039103001206
                  2. NMB
                    MTWANGO SECONDARY SCHOOL
                    ACCOUNT NO.6063500087
                   3. CRDB
                     MTWANGO SECONDARY SCHOOL
                     ACCOUNT NO.0150349760200
            Pembeni  kwenye  “pay  in  slip”andika  ada  ya………………..(jina  la  mwanafunzi).Unaporipoti  uje  na  hiyo”pay  in  slip”.

 ………….MKUU WA SHULE………………Tarehe





















            REQUEST FOR MEDICAL   EXAMINATION

PART A:
TO THE MEDICALOFFICER
…………………………………………..
…………………………………………..
…………………………………………..
…………………………………………..
                                                                              FROM THE HEADMASTER
                                                                             MTWANGO SECONDARY SCHOOL
                                                                               PO BOX 370
                                                                                NJOMBE.
RE: Mr/Miss………………………………………………………………………………..
Please examine the above named as to her or his fitness for  admission as a student at mtwango secondary school
                                                                        Date……../……../…….

                                                                        Signature………………..

                                                                         Stamp……………………

PART B:

MEDICAL CERTIFICATE
(To be  completed  by the medical officer)
I have examined the above mentioned and consider that he/she is physical fit /unfit for admission as a student to the said school.

Date…….../……/…..                                        Signature………………………

Station……………..                                          Designation…………………….

                                                                            Stamp………………………….













WIZARA YA   ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
          SHULE YA   SECONDARY MTWANGO

                       
                     SHERIA ZA SHULE
Kila mwanafunzi lazima asome shelia hizi kwa uangalifu azielewe,azifuate na kuzitii.
Uvunjaji wa sheria  yoyote ya shule hata kama ni ndogo kiasi gani hauta vumiliwa katika shule hihi na shirika la NDDT kwa ujumla.

  MAKOSA YANAYO WEZA KUSABABISHA KUFUKUZWA SHULE
Makosa yafuatay yana weza kusababisha mwanafunzi kufukuzwa shule mara moja.
1. Wizi wa aina yoyote
2. Uasherati
3. Ulevi wa aina yoyote
4. Uvutaji bangi
5. Makosa ya jinai
6.Kupigana
7. Kuharibu Kwa makusudi Mali ya umma
8. Utolo shuleni
9. Kudharau bendera ya Taifa
10. Kutofanya mtihani    wowote unaoandaliwa na shule
11. Kutotii ratiba ya shule
12. Kusababisha au kushiriki katika migomo
13. Kumiliki simu ya mkononi ukiwa shuleni

MENGINEYO
1. Unatakiwa kuvaa mavazi rasmi ya shule wakati wote
2. Hutakiwi kukaa na madawa bwenini bila idhini.
3. HURUHUSIWI KUWA NA SIMU SHULENI.NI MARUFUKU
4Unatakiwa kula chakula kilicho andaliwa na shule.